KIUNGO wa zamani wa timu ya Barcelona, Xavier Hernandez ‘Xavi’, amesema haoni sababu ya kocha wake wa zamani ambaye kwa sasa anafundisha timu ya Manchester City, Pep Guardiola, kushindwa kutwaa michuano ya Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu England msimu huu.
Kauli hiyo ya Xavi inatokana na mafanikio ya kocha huyo aliyoyapata akiwa Barcelona na Bayern Munich na  baadaye kujiunga na timu ya Manchester City inayoonekana kuanza vema katika michuano mbalimbali inayoshiriki msimu huu.
Guardiola amekuwa  na mwanzo  mzuri katika klabu hiyo ambapo hadi sasa  amefanikiwa kushinda michezo mitano ya  Ligi Kuu England na  mchezo mmoja wa Ligi  ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Monchengladbach.
Xavi  anaamini kocha huyo huenda akapata  mafanikio makubwa akiwa katika klabu hiyo na kusisitiza kwamba  msimu huu anaweza kushinda kila kitu katika michuano anayoshiriki.
“Guardiola ni bingwa, atahitaji  kushinda  makombe yote msimu huu  akiwa na kikosi chake Manchester City na hakuna sababu ya kushindwa kufanya hivyo. Ameshinda  mataji matatu akiwa Barcelona na anaweza kushinda zaidi ya hapo  msimu huu, taji la Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Ulaya ni maalumu lakini kwa tamaa aliyonayo atahitaji kushinda kila kitu.
“Manchester City hawana kikosi cha pili, hata hivyo si jambo jema kuwaita hivyo kwani inawezekana kocha Guardiola akafanya mabadiliko katika baadhi ya michuano wanayoshiriki, hicho ndicho kitakachofanyika kwani hawezi kushinda  mataji akiwa na kikosi cha wachezaji 11 tu na kutarajia kushinda kila taji,” alisema Xavi.
Hata hivyo,  Xavi alisema licha ya mwanzo mzuri wa timu hiyo, aliwaonya wachezaji wa timu hiyo  kutokukata tamaa wakiwa na kocha huyo hadi hapo watakapokuwa mabingwa.
“Manchester City tayari wamekuwa vinara wa Ligi Kuu England lakini najua Guardiola hatahitaji mzaha katika vyumba vya kubadilishia nguo,” alisema Xavi.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours