Kampuni ya Yahoo imethibitisha kuwa akaunti milioni 500 za wateja wake zimeibiwa, jambo ambalo ni la uvunjifu wa sheria.
Kampuni hiyo imesema ina amini kuwa zoezi hilo limefanywa mwaka 2014 na Serikali kwa dhumuni lakukusanya data muhimu katika akuti hizo.Yahoo imewasihi watumiaji wake kuwa makini lakini pia kubadilisha namba za siri ili kuhakikisha taarifa zao zinazopatikana kupitia namba zao za simu, anuani, tarehe, siku, miaka pia maeneo yakuzaliwa na nynginezo hazichukuliwi.
Kwa upande mwingine, Yahoo imesema hakuna taarifa zozote zilizoweza kuibiwa kupitia akaunti na kadi za kielektroniki za benki.
Hata hivyo, kwasasa Yahoo kwa kushirikiana na Vyombo vya Sheria kufahamu zaidi kilichotokea. (Source BBC)
0 comments so far,add yours