KUTOKANA na kushuka kwa kiwango cha elimu mkoani Dodoma, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana,  ametoa siku 14 za kukutana na wakuu wa wilaya zote, wakurugenzi wote, maofisa elimu na viongozi wa Chama cha Walimu (CWT) ngazi zote, kufanya kikao cha pamoja ili kupata ufumbuzi wa kupandisha kiwango cha elimu mkoani hapa.
Agizo hilo alilitoa juzi, wakati akifungua warsha iliyoandaliwa na baraza la walimu kitengo cha wanawake kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali.
Pia amelitaka Baraza la Walimu Kitengo cha Wanawake Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa kuboresha elimu kwa watoto wa kike, hususan wanaotokana na mazingira magumu na hatarishi.
Alisema ili kufanikisha sera ya elimu bure, lazima kiwango cha ufaulu kiongezeke shuleni, hususan katika Mkoa wa Dodoma.
Alisema hajafurahishwa na matokeo ya mkoa huo, kwa  kuwa nyuma kielimu, badala ya kushika nafasi nzuri yenye hadhi ya kuwa makao makuu.
“Sijapendezwa hata kidogo kuona Mkoa wa Dodoma unakuwa nyuma kielimu kutokana na hali ya sasa ya sera ya serikali ya elimu bure, lazima kuwapo na mikakati ya kukuza elimu kwa vijana wetu,” alisema Rugimbana.
Kwa upande wake, mwakilishi wa baraza hilo, Renatha Simbachawene, alisema kushuka kwa elimu ni changamoto ambazo zinasababishwa na wazazi kutokuwa karibu na walimu.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours