HIVI karibuni Rais wa Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta alikuwa
ziaraniUchina na katika mikataba aliyosaini ni pamoja na ule wa ujenzi
wa reli toka Malabo hadi Mombasa, hii ikiwa na maana Uganda haina
tenampango wa kupitisha mizigo yake huko Tanga.
Chokochoko zetu na Rwanda na Malawi kwa kiasi
fulani zinazikimbiza nchihizo kuing’ang’ania Kenya au Msumbiji, kama
njia yao kuu ya usafirishaji na siyo Tanzania.
Siasa zisizoangalia maslahi ya nchi na watu wake,
binafsi, ninaamini siyo siasa zenye mwelekeo sahihi. Baadhi ya misimamo
na mitazamo tuliyoichukua ingelifaa ipitiwe upya na sisi wenyewe
kujirudi kwa kuangalia masilahi ya muda mrefu ya nchi na watu wake.
Tanzania ni nchi kubwa, lakini isitumie ukubwa wake kuwafanya wengine
kujiona wadogo na watu wasiyo na thamani.
Tukifanya hivyo, tutakuwa na kazi kubwa ya kuwa na
marafiki wa kweli miongoni mwa nchi jirani zinazotuzunguka. Siyo vyema
wanasiasa wetu pia kukurupuka na kuingiia mambo ya kidiplomasia.
Tungewaachia wanadiplomasia wao wenyewe waifanye kazi waliyoisema na wanayoijua.
Hatuwezi kuilaumu Kenya kwa kutaka kuiokoa bandari
yake ya Mombasa na vilevile hatuwezi kugombana nao kuhusu uamuzi wao wa
kujenga bandari mpya kule Lamu.
0 comments so far,add yours