Dodoma
Kambi ya Upinzani Bungeni imeishauri serikali kutojiingiza katika usimamizi na uendeshaji wa shughuli za ushirika nchini, kwa kuwa hatua hiyo inaenda kinyume na misingi ya ushirika na inaondoa mamlaka ya wanaushirika.
Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo bungeni mjini Dodoma, kufuatia
kuwasilishwa kwa muswada wa sheria ya vyama vya ushirika, mbunge wa viti
maalum (CHADEMA) Bi. Rose Kamili Sukum, amesisitiza kuwa serikali
haiwezi kuwa mtendaji mkuu kwenye ushirika, kwa kuwa utendaji wa
ushirika hauna tofauti na sekta binafsi.Kambi ya Upinzani Bungeni imeishauri serikali kutojiingiza katika usimamizi na uendeshaji wa shughuli za ushirika nchini, kwa kuwa hatua hiyo inaenda kinyume na misingi ya ushirika na inaondoa mamlaka ya wanaushirika.
Nayo, Kamati ya bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake, Mbunge wa Sikonge, Bw. Said Nkumba, imetaka kufutwa kwa chama kilele cha ushirika, kwa kuwa kinaongeza mzigo kwa wanaushirika.
Aawali akiwasilisha muswaada huo wa sheria ya vyama vya ushirika nchini, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Eng. Christopher Chiza, amesema kutungwa kwa sheria hiyo, kumetokana na azma ya serikali kufufua na kuimarisha sekta ya ushirika nchini.
0 comments so far,add yours