Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Prof.Jakaya Mrisho Kikwete amesema miradi mingi ya maendeleo inayotegemea misaada ya kisayansi kutoka katika nchi zilizoendelea hukwama kwa nchi hizo kusitisha misaada pale nchi masikini tanzania ikiwemo zinapokataa kutekeleza matakwa ya nchi hizo hivyo ni vyema nchi masikiini zikawa na mkakati maalum wa kuanza kuwekeza katika nyanja za kisayansi.
Rais Kikwete ameitoa kauli hiyo jijini Dar es salaa, katika
harambee ya kuchangia ujenzi wa chuo kikuu cha tumaini kampasi ya Dar es
salaam na kuongeza kuwa taifa lolote linalotegemea misaada kutokanje ya
nchi haliwezi kuwa na maendeleo endelevu kwani nchi masikini
zinapotofautiana na matakwa ya nchi zinazotoa misaada hususan ya
kisayansi husitisha misaada yao na hivyo kukwamisha maendeleo ya nchi
husika.
Rais kikwete amezitaka taasisi na vyuo vikuu vya hapa nchini
kuendelea kuimarisha miundo mbinu ya kujifunzia hususani ya kisayansi
ili kuondokana na kadhia ya kutegemea misaada ya kisayansi kutoka katika
nchi zilizoendelea kwa kuwekeza katika sekta ya elimu ili kupata
wataalam watakaosaidia maendeleo ya nchi.
Kwa upande wake askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheri
tanzania KKKT, ASKOFU ALEX MALASUSA ameishukuru serikali kwa jitihada
zake za kusaidia wananchi wa hali ya chini ili waweze kupata elimu ya
juu kwa kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wote wenye sifa na
kwamba kanisa hilo litajitahidi kuendelea kuchangia katika sekta ya
elimu kupitia taasisi zake za elimu.
0 comments so far,add yours