PATRICIA KIMELEMETA NA CHRISTINA GAULUHANGA
SIKU mojaa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu kuwaamibia wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi la hivi karibuni mkoani humo, wajitegemee na kwamba misaada yote iliyotolewa ni ya Serikali na taasisi zake tu, kauli hiyo imewashangaza viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Katibu wa Taifa wa chama hicho, Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Janeth Rithe ilisema kauli hiyo haikubaliki kwa sababu inadhalilisha waathirika na taasisi zote zilizojitokeza kuwasaidia waathirika hao.
Alisema chama hicho kimeshtushwa na kauli hiyo na kuichukulia kama ni tangazo halali la wizi wa uaminifu wa mali za wananchi zilizotolewa na taasisi mbalimbali kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo.
“Kauli iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu, Salum Kijuu, hatuwezi kuiunga mkono kwa sababu inadhalilisha waathirika wa tetemeko la ardhi.
“Ikumbukwe tangu tetemeko hilo litokee, taasisi na wananchi mbalimbali walijitokeza kuwasaidia waathirika hao, kwa nini sasa wanashindwa kupewa mali zao na badala yake zinatoka kauli kama hizo? Hatuwezi kuunga mkono,”alisema Janeth.
Alisema ni busara ya kawaida kuwa hatua ya kwanza katika kushughulikia maafa ni kurudisha hali ya maisha ya watu katika hali ya kawaida sambamba na ukarabati wa miundombinu.
Alisema suala la ujenzi wa miundombinu ya taasisi za umma, ni jukumu la msingi la Serikali ambalo haiwezi kulikwepa.
Alisema chama hicho kimeitaka Serikali kuu kujitenga na kufuta kauli ya mkuu wa mkoa wa Kagera kwa sababu inaweza kusababisha migongano baina ya wananchi na serikali yao.
Serikali inapaswa kuelekeza misaada iliyotolewa ikiwamo michango kwa waathirika wa tetemeko hilo kama ilivyokusudiwa, alisema.
Rithe alisema chama hicho kimetoa wito kwa taasisi za raia nchini kuchukua nafasi yake katika kuendelea kuikumbusha serikali wajibu wake wa msingi wa kuboresha maisha ya watu.
Alisema Watanzania wanakumbuka Septemba 10, 2016 lilitokea tetemeko la ardhi Kanda ya Ziwa na hususan Mkoa wa Kagera, ambalo lilisababisha baadhi baadhi ya wananchi kufariki na wengine kulazwa, huku nyumba na mali zao zikiharibika vibaya.
“Tetemeko hilo lilisababisha athari mbalimbali vikiwamo vifo, majeruhi, uharibifu wa makazi na miundombinu ya umma na watu binafsi, takwimu zilizotolewa na mkuu wa mkoa huo, zilionyesha watu 117,721 waaliathirika kwa kupoteza makazi yao,”alisema.
Alisema nyumba 2,072 za makazi zilianguka na 14,595 zilibomoka, baadhi zilipata nyufa hivyo kuzifanya kuwa hatarishi kwa makazi ya binadamu.
Kutokana na hali hiyo, taasisi mbalimbali, nchi marafiki, waliitikia wito wa kuwasaidia waathirika wa maafa na kukarabati miundo mbinu iliyoharibika, alisema.
“ Hadi kufikia Oktoba, mwaka huu, f edha, vyakula na vifaa mbalimbali vya ujenzi vilikuwa vimepatikana kwa njia ya michango mbalimbali,”alisema.

0 comments so far,add yours