Kufuatia tukio la watu wenye imani za kishirikina kumkata mkono mtoto
mwenye ulemavu wa ngozi albino huko mkoani Tabora mmoja wa waganga wa
jadi hapa nchini Athuman Kaita ameiomba serikali kuwasaka na kuwakamata
wahusika wote wa tukio hilo na kuwachukulia hatua kali za kisheria ili
kukomesha unyama huo.
Akizungumza na ITV mkoani Iringa bwana Athuman Kaita maarufu kama
dokta ngoma nzito amesema ni vema serikali ikafanya uchunguzi wa kutosha
na kuwashughulikia wahalifu hao kama wahalifu wengine kwani unyama huo
ni uhalifu kama ulivyo uhalifu mwingine.
0 comments so far,add yours