Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amethibitisha
kukamatwa kwa watu hao ambapo amesema watuhumiwa walikamatwa katika
eneo la kola kwa kamnyonge manispaa ya Morogoro wakihujumu miundombinu
ya umeme ikiwemo kuiba mafuta ya trasfoma na kukata nguzo za umeme
ambapo jeshi la polisi linaendelea kuwahoji watu hao na mara baada ya
upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani.
Naye afisa uhusiano wa shilika na umeme Tanesco mkoa wa Morogoro
Ester Msaki amsema mafuta hayo yana thamini ya zaidi ya shilingi laki
tatu ambapo amewataka wananchi kuendelea kuwa na ushirikiano kwa
kuwafichua wanaohujumu miundombinu ya umeme kwani shirika linaendelea
kupata hasara na kusababisha baadhi ya wananchi kukosa huduma ya umeme.
Kwa upande wao wakazi wa manispaa ya Morogoro wameiomba serikali
kuongeza ulinzi na kuwachukilia hatua kali watakaobainika wakihujumu
miundombinu ya umeme na kusababisha wananchi kuishi gizani kwakukosa
huduma ya umeme.
0 comments so far,add yours