Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Waziri Nyanga (30) mkazi wa
Tandika Dar es salaam anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kukutwa
na nyaraka mbalimbali za shirika la maji safi na maji taka Dawasco huku
akifanya kazi za kukatia wananchi maji na kukusanya mapato.
Mtu huyo alikutwa na nyaraka hizo zikiwamo Tisheti, Kofia, Karatasi
mbalimbali pamoja na stakabadhi na vifaa vya kukatia maji endapo
mtumiaji wa maji hakulipa bili huku akikosa uhalali wa kufanya hivyo
kwakuwa hatambuliki na uongozi wa Dawasco na pia hakuwa na kitambulisho
kinamchomtambulisha kuwa ni mfanyakazi wa shirika hilo.
Uchunguzi uliyofanywa ulibaini mtuhumiwa alikuwa akifanya shughuli
hizo kwa miaka mitatu na alikuwa akitoa stakabadhi kwa waliyolipa na
kukata maji kwa waliyokosa fedha na alipopekuliwa nyumbani kwake
alikutwa na nyaraka hizo na kufikishwa kituo cha polisi Chang'ombe.
0 comments so far,add yours