Mkuu wa wilaya ya Karatu mkoani Arusha Bw Felexs Ntebenda
amewatakata wananchi wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano wa kuwezesha
kukamatwa kwa kikunadi cha watu kinachoendesha vitendo vya hujuma
kwenye miradi ya maji na umeme inayotekelezwa katika maeneo mbali mbali
ya wilaya hiyo.
Bw Ntebenda ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi
wa kata ya Endamarieki juu ya kuwepo kwa watu wanao haribu
miundombinu ya maji na kuhamasisha wananchi kudai fidia zisizo za
lazima kwenye miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao.
wakizungumzia changamoto hiyo baadhi ya viongozi akiwemo mbunge
wa karatu Mh Israel Natse wamewataka wananchi kutambua kuwa miradi
yote inatekelezwa kwa kodi zao hivyo wanapoona mtu anaharibu anachezea
fedha na nguvu zao.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema miradi mbalimbali
ikiwemo ya ,maji na umeme inayotekelezwa kwenye maeneo yao imeanza
kuwapunguzia makali ya maisha.
0 comments so far,add yours