PATRICIA KIMELEMETA
UKATILI wa ngono bado ni tatizo nchini ambako zaidi ya asilimia 80 ya wanawake wamefanyiwa katika   mwaka mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari   Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Rehema Msami alisema takwimu zilizoripotiwa mwaka jana zilionyesha kesi za ukatili wa  ngono zilikua 245.
Alisema matukio hayo yalitokea katika Wilaya za Muleba, Kasulu na Kinondoni.
Msami alisema  juhudi za haraka zinahitajika  kutoa elimu kwa wananchi hali ambayo inaaminika, inaweza kupunguza ukubwa wa tatizo hilo.
“Vitendo vya ukatili wa ngono bado vinaendelea nchini. Hadi sasa ni zaidi ya asilimia 80 ya wanawake wamefanyiwa vitendo hivyo.
“Hali inayoonyesha wazi kuwa juhudi za haraka za kushirikiana na wadau mbalimbali kutoa elimu zinahitajika,” alisema Msami.
Alisema pamoja na ukatili huo,   pia kesi za ukatili wa jumla zilifikia 6,853   mwaka jana pekee.
Alisema kutokana na hali hiyo, serikali inapaswa kushirikiana na wadau mbalimbali  waweze kuangalia namna ya kupunguza vitendo vya ukatili nchini.
“Tunapaswa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwamo viongozi wa dini na serikali   kuangalia namna ya kutoa elimu kwa wananchi  waweze kuondokana na ukatili,” alisema.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours