serikali inaangalia uwezekano wa kuanza kuwatumia vijana wa skauti katika vyombo vya ulinzi na usalama huku ikiwaagiza wakurugenzi wa halmashauri kuwaruhusu walimu kushiriki katika shughuli za skauti.
Hayo yameelezwa na Rais DR. JOHN POMBE MAGUFULI katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa DKT HUSEIN MWINYI na pia kuagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinavilinda kikamilifu vyama vya skauti ili visife bila sababu za msingi.
Rais wa Skauti Tanzania Profesa JOYCE NDALICHAKO ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi licha ya kupongeza juhudi kubwa zinazofanywa na uongozi mpya wa skauti kukiimarisha chama hicho, amesema ni vema chama kikaangalia uwezekano wa kuongeza wigo wa kuwapata vijana wengi zaidi.
Akitoa maelezo ya utendaji kazi wa chama hicho tangu uanze uongozi mpya mwaka 2013, Kamishina Mkuu wa Skauti Tanzania ABDULKARIM SHAH amesema kazi kubwa wanayoifanya kwa sasa ni kuhakikisha wanarejesha heshima ya chama hicho iliyokuwa imepotea kwa miaka kadhaa.
0 comments so far,add yours