Wananchi waliokuwa wamepiga kambi porini kwa madai ya kuondolewa kwenye maeneo ya hifadhi wameanza kuondoka baada ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Babati kuwakamata baadhi ya watu wanaodaiwa kuchochea mgogoro huo wakiwemo viongozi wa kata na tarafa.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Babati Bw Chrispin Meela amewataja walikamatwa kuwa ni pamoja na afsa tarafa ya mbugwe Bw Gitu Sedoyeka, na diwani wa kata ya kiasangaji Bw Adamu Isingika (CCM) walikokusanyika wananchi hao hatua hiyo imekuja baada ya viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo mbunge wa viti maalumu mkoa wa Manyara Mh. Anna Joram kuwatembelea wananchi hao na kuwasihi waondoke ushauri ambao hata hivyo waliukataa.
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya Bw Meela Nusu ya kundi la wananchi hao wameshaondoka na taratibu za kuwaondoa wengine zinaendelea sambamba na kuwatafuta viongozi wengine wanaodaiwa kuchochea mgogoro huo wakiwemo ambao wameshakamatwa, na wanadaiwa kutumiwa na baadhi ya watu wenye uwezo mkubwa kifedha.
0 comments so far,add yours