Wananchi kumi na sita elfu wa kijiji cha Libango wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wanakosa huduma muhimu baada ya daraja la Libango linalounganisha kijiji hicho na makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kuharibiwa na mvua huku wakazi zaidi ya laki mbili wa wilaya ya Namtumbo wakikosa mawasiliano na kijiji hicho.
Wakazi wa kijiji cha Libango wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wanasema kuwa maisha yamekuwa magumu baada ya daraja hilo la Libango ambalo liko katika mto Lwegu kuharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha kwani mawasiliano kati ya kijiji hicho na makao makuu ya wilaya ya namtumboi yamekatika huku vijana wakijipatia ajira ya kuwavusha watu kwa shilingi elfu mbili.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Libango Bw.Christopher Ngonyani alinusurika kuzama kwenye mto Luegu ambapo ndipo pana dara la Libango wakati akijaribu kuvuka katika mto huo ili awahishe nyaraka za kiofisi kwenye ofisi za halamashauri ya wilaya ya Namtumbo.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Bw.Chande Bakary Nalicho ametembelea eneo la tukio na kupiga marufuku kuvusha watu kwa kutumia miti huku akisema watajenga daraja la muda wakati juhudi za kulijenga daraja hilo zikifanyika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments so far,add yours