Baadhi ya wananchi wa eneo la Mloganzira Kwembe jijini Dar es Salaam wamevamia ofisi za wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi wakishinikiza kulipwa madai yao ya fidia baada ya kupisha mradi wa chuo cha muhimbili na kusababisha shughuli za wizara hiyo kusimama kwa muda.
Wananchi hao wamevamia ofisi hizo huku wakiimba nyimbo mbalimbali
zilizokuwa zikishinikiza kulipwa madai yao ambapo wamedai kuwa tangu
waondoke kwenye maeneo yao kupisha mradi ni zaidi ya miaka kumi
hawajalipwa licha ya Rais kuwaahidi kuwa hawataachwa bila kulipwa.
Kufuatia hali hiyo naibu waziri wa wizara hiyo Mh. Anjela Kairuki
amelazimika kutoka ofisini na kuzungumza na wananchi hao ambapo
amekutana na wakati mgumu kwani kila alipotaka kuzungumza nao baadhi yao
walionekana kutoridhishwa na majibu yake na kuanza kumzomea, na baade
aliweza kuwatuliza kwa kuwaeleza kuwa ndani ya siku saba watakwenda eneo
husika kuzungumza nao.
Hata hivyo licha ya Mh.Kairuki kutoa kauli hiyo baadhi ya wananchi
wamemweleza kuwa wakati wanamsubiri wanarudi kwenye maeneo yao huku
wakitishia kusimamisha mradi hadi watakapolipwa fedha zao, ambapo
kutokana na hali hiyo polisi walionekana kutanda katika eneo la wizara
ya hiyo huku wengine wakiwa na silaha za moto.
0 comments so far,add yours