Wananchi wa kata ya Nyankende katika
wilaya ya kahama mkoani Shinyanga wameitaka serikali kutafuta mbinu za
kupandisha bei ya pamba zao ambalo linategemewa katika shughuli zote za
kimaendeleo hali inayotishia kuporomoka kwa uchumi katika mkoa wa
shinyanga na kuwafanya wananchi kuishi maisha duni na ya dhiki.
Hayo yamesemwa na diwani wa kata ya Nyankende wilayani kahama Mh.
Doa Limbu kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa hadhara
ulioitishwa na mkuu wa mkoa wa shinyanga ili kujadili changamoto
zinazowakabili wananchi hao ambapo kata hiyo haijawahi kutembelewa na
mkuu wa mkoa yeyote tangu ianzishwe.
Naye mkuu wa wilaya ya kahama Bw.Benson Mwampesya amewataka
wananchi wa kata ya Nyankende kulima mazao mengine ya biashara na
chakula ikiwemo zao la alizeti kwakuwa kuanguka kwa bei ya zao la pamba
sio swala la tanzania pekee na hakuna namna ya kupandisha bei ya zao
hilo kwa haraka.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa shinyanga Bw.Ally Nasoro Rufunga
amewaahidi wananchi hao kuwaletea wawekezaji watakaoingia ubia katika
kilimo cha mkataba hali itakayosababisha kukua kwa sekta ya kilimo
katika kata hiyo.
0 comments so far,add yours