Wakazi wa nyumba zaidi ya mia moja na
hamsini zilizokamilika na zilizo katika ujenzi kwenye eneo la vikongoro
-CHANIKA wamejikuta wakipoteza makazi yao baada ya nyumba hizo kuvunjwa
na serikali wilaya ya ilala kwa kudaiwa kuwa ni wavamizi.
Ni sehemu ya wakazi wa eneo hilo la vikongoro wakipaza sauti zao
mara baada ya ITV kufika eneo la tukio kushuhudia kilichotendeka ambapo
wakazi hao wamesema wamevunjiwa nyumba zao pamoja na zile walizokuwa
wakiendelea kujenga ilhali wanamiliki maeneo hayo kihalali.
Mmoja kati ya wakazi wa eneo hilo EFESO MSEMO amesema vijana
waliohusika na kufanya uvunjaji huo walikuwa wakichukua vitu
walivyokuwa wakikuta ndani ya nyumba hizo sambamba na kunywa vinywaji
walivyokuwa wakikuta katika maduka wanayoyavunja.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo ameiambia ITV kwa njia ya simu
kuwa alipewa taarifa na kamanda wa polisi wa wilaya ya kipolisi ya
ukonga kuwa uvunjaji huo unatokana na wakazi hao kuvamia katika eneo
ambalo linamilikiwa kihalali na mtu mwingine.
0 comments so far,add yours