Wananchi wa kata ya msanga mkuu wilaya ya mtwara vijijini
wamelazimika kurudia usafiri wa mitumbwi baada ya kivuko kilicholetwa
na serikali miezi miwili iliyopita kusitisha safari zake baada ya
kugonga mwamba na kuvunja gia.
Akizungumzia tatizo hilo kaimu meneja wa wakala wa ufundi na umeme
tamesa mkoa wa mtwara Elitraudi Mmbemba amesema tatizoli hilo
limetokana na upepo mkali na hivyo nahodha kukosa mwelekeo na kugonga
mwamba.
Hata hivyo amesema hakuna abiria aliyepata tatizo kuhusiana na
tukio hilo na tayari kifaa hicho kimemepatikana jijini Dar es salaam na
wakati wowote kitawasili na kufungwa ili kiendelee na kazi kama
kawaida.
Wakizungumzia adha ya kurudia usafiri wa mitumbwi baadhi ya
wananchi wa msanga mkuu ambao sehemu kubwa ya maitaji huyapata mtwara
mjini wamesema kifaa hicho kiharakishwe mapema kufungwa kusudi waandelee
na usafiri wao kama kawaida kuliko wanaoutumia wa mtumbwi ambao
hauaminiki asilimia kubwa.
kivuko hicho hutumia muda wa dakika 15 kuvusha watu kutoka gati ya mtwara kuelekea ghati ya msanga mkuu.
0 comments so far,add yours