Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr. Reginald Mengi amesema iwapo serikali
itaandaa mazingira mazuri vijana na Watanzania kwa ujumla wanaweza
kujikwamua kiuchumi kwa kutumia akili, juhudi, na utajiri wa raslimali
za taifa.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP DR Reginald Mengi ameyasema hayo jijini
Dar es salaam wakati akizindua shindano jipya la kubuni Wazo la Biashara
litakaloendeshwa kwa miezi sita mfululizo kuanzia Januari 2015, na kila
mwezi mshindi mmoja atajishindia zawadi ya shilingi milioni 10
atakazozitumia kama mtaji wa kutekelezea kwa vitendo wazo lake la
biashara.
Amesema Shindano hilo linalojulikana kama 3N ikiwa ni kifupisho cha
‘NITABUNI biashara, NITATEKELEZA na NITAFANIKIWA’, litawashirikisha
Watanzania pekee na litaendeshwa kwa njia ya mtandao wa kompyuta ambapo
mshiriki anatakiwa atatume wazo lake kwa anuani ya twita @regmengi
shindano la wazo la biashara.
Katika kupata mshindi, jopo maalum la wataalamu watapitia mawazo
yatakayowasilishwa na kuteua mawazo 10 bora, na watunzi wa mawazo hayo
10 watafanyiwa usaili kwa njia ya simu ili jopo lijiridhishe kuwa mawazo
waliyotoa ni yao binafsi na jinsi walivyojiandaa kuyatekeleza
kibiashara. Jopo la wataalamu litamteua mshindi baada ya usaili huo.
0 comments so far,add yours