Nyumba ambazo idadi yake haijaweza kufahamika mara moja zimebomoka na zingine kuingiwa na maji, miti kuanguka ovyo huku pia baadhi ya barabara katika manispaa ya Mtwara/mikindani zikijaa maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Mtwara.
ITV ilifika kwenye eneo la magomeni bomba la bure na kukuta baadhi
ya wakazi wake wakihangaika kuyatoa maji yaliyoingia ndani ya makazi yao
kutokana na mvua hiyo kunyesha siku mzima kuanzia usiku wa manane, huku
maeneo mengine yakishuhudiwa wakazi wake wakihangaika kuhamisha vifaa
vya ndani kuyakimbia mafuriko hayo.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo la Magomeni Bomba la bure wamedai
wamepata hasara kubwa kutokana na mafuriko hayo na kwamba yanasababishwa
na barabara mpya ya chuno kuelekeza mifereji yote ya maji kwenye
makazi yao na hakuna jitihada zo zote za serikali kuwasaidia kuondokana
na tatizo hilo.
Kwenye maeneo ya Skoya na Kyanga ITV ilishuhudia barabara
zimefunikwa na mafuriko na magari yakipita kwa taabu huku wakazi wa
maeneo hayo wakiiomba serikali kuwalipa fidia ya hasara na mali zao kwa
kuwa mafuriko hayo yamekuwa yakijirudia rudia na serikali imeshindwa
kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.
0 comments so far,add yours