Jitihada za Tanzania za kusaidia kuleta ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa katika nchi ya Sudani kusini kwa njia mazungumzo umeanza kuonyesha mwelekeo wa mafanikio baada ya viongozi wa makundi matatu yaliyotofautianandani ya chama cha (SPLM) kusaini makubaliano ya kusitisha mapigano na kuanza mazungumzo.
Wakizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo mbele ya marais Mh.
Uhuru Kenyeta wa Kenya, Yoweri Museven wa Uganda na mwenyeji wao Mh Rais
Dr, Jakaya Kikwete viongozi makundi yote yaliyotofautiana wameahidi
mbele ya marais Dr, Jakaya Kikwete wa Tanzania, kuheshimu makubaliano
yaliyofikiwa.
Kwa upande wao rais Uhuru Kenyata wa Kenya na Yoweri Museveni wa
Uganda wamewataka viongozi wa makundi hayo kuona umuhimu wa kutanguliza
mbele maslahi ya wananchi wao wanaoendelea kuteseka kwa sababu ya
tofauti za mitazamo ambazo zinaweza kumalizika bila kupigana, na
wameipongeza Tanzania kwa kuendeleza harakati za hayati baba wa taifa
Mwalim Nyerere za kumaaliza matatizo kwa njia za mazunguzo.
Awali mwenyekiti wa mazungumzo hayo Mh John Malechelea na katibu wa
CCM iliyokuwa inaratibu zoezi hilo Mh Abdulrahaman Kinana pamoja na
kueleza baadhi ya makubaliano yaliyofikiwa na pande zote likiwemo la
kuheshimu uhuru na haki kila mwanachama kugombea nafasi za uongozi
wamewataka viongozi hao kuwa na uvumilivu wa kisiasa.
Akihitimisha kikao hicho rais wa Tanzania Mh Dr, Jakaya Kiwete
amesema Tanzania itanedelea kutoa mchango wake wa hali na mali wa
kupigania amani na kuhakikisha mazungumzo yanatumika kumaliza tofauti
popote zinapojitokeza kwani ni jambo linalowezekana.
0 comments so far,add yours