Bunge limechachamaa na kutaka
serikali ianze kuchukua hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na
kuwakamata, kuwashtaki na kuwafilisi wale wote wanaohusika katika
ubadhirifu na upotevu wa fedha za serikali kutokana na kukosa uzalendo
na uwajibikaji badala ya kila mwaka bunge kupokea ripoti ya ubadhirifu
unaosababishia taifa hasara ya mabilioni ya shilingi na kwamba kujiuzulu
ama kufukuzwa kazi pekee si suluhisho ili kuwa na taifa lenye nidhamu
katika matumizi ya fedha za umma.
Bunge limepata fursa ya kuzijadili taarifa za kamati ya bunge ya
hesabu za serikali ambayo taarifa yake inaonesha kuwa zaidi ya shilingi
bilioni 100 zimekwepwa kulipwa na makampuni mbalimbali kwa kivuli cha
misamaha ya kodi na takribani bilioni 8 nazo zikipotea baada ya mamlaka
ya bandari kufanya manunuzi ya dharura bila kibali cha mlipaji mkuu wa
serikali jambo liliwafaanya baadhi ya wabunge kugeuka mbogo.
Hata hivyo wakati majadiliano yakiendelea kukaibuka mabishano ya
kisheria dhidi ya mh Tundu Lissu na mwanasheria mkuu wa serikali Ndg
George Mcheche Masaju baada Mh Lisu kutaka rais awawajibishe baadhi ya
majaji waliohusika katika sakata la Tegeta Escrow kwa kuwa katiba inampa
mamlaka huku ndg Masaju akiliambia bunge tume ya utumishi wa mahakama
kwa mujibu wa katiba ndio inapaswa kumshauri rais juu ya masuala ya
nidhamu za majaji.
Kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni kuepuka kuingilia mihimili
mingine hasa mahakama baaadhi ya wabunge wameonesha kutoridhika na hoja
hiyo kutokana na wabunge kuzuiwa kulijadili sakata la uda kutokana na
taarifa za uwepo wa kesi kadha wa kadha mahakamani zinazohusu uda baada
ya mwanasheria mkuu wa serikali kushauri kutojadiliwa bungeni kutokana
na kamati ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa kuitaka serikali kutoa
maelezo bungeni endapo ni kweli hisa za uda zimeuzwa kwa kampuni
binafsi ya simon group limited ama la.
Mara baada ya muongozo huo mwenyekiti Mh Musa Azan Zungu akaitaka
kamati uongozi ya bunge kukutana ili kulijadili suala hilo kwa madai
kuwa kuna mambo yako mahakamani na mengine hayapo mahakamani lakini
bunge linakosa fursa ya kuyajadili.
0 comments so far,add yours