Chama cha demokrasia wilayani Iringa kimelalamikia rafu na kasoro
mbalimbali zilizojitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa
uliofanyika Disemba 14 nakusema kuwa uchaguzi huo uligubikwa na kasoro
nyingi ambapo wakati uchaguzi huo ukiendelea hii leo watu wasiojulikana
wamemshambulia kwa nondo na mapanga katibu wa mbunge wa Iringa mjini
Bwana Joseph Mgima.
Akizungumza kwenye mahojiano na ITV Bwana Mgima amesema tukio hilo
lilitokea usiku wa jana majira ya saa mbili usiku wakati alipokuwa
akienda kuzungumza na mawakala wa chama chake kwenye mtaa wa Bwawani
kata ya Mkwawa ndipo alipokutana na watu hao waliokuwa kwenye bajaji
mbili ambapo mmoja wa watu hao alimpiga teke na kuangukia mtaroni ndipo
watu wengine sita kutoka kwenye hizo bajaji walipoanza kumpiga kwa
mapanga.
Mwenyekiti wa baraza la vijana la chaama cha demokrasia na
maendeleo Chadema wilaya ya Iringa Leonce Marto amesema tukio hilo
linauhusiano mkubwa na uchaguzi wa marudio wa wenye viti na wajumbe
katika mitaa 19 katika manispaa ya Iringa akiwatuhumu wapinzani wao wa
CCM kutumia mbinu chafu kushinda kwenye mitaa hiyo huku kamanda wa
polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi akisema jeshi hilo linachunguza
tukio hilo na litawashughulikia wote watakaobainika kufanya uhalifu huo.
Zoezi la uchaguzi linafanyika hii leo ikiwa ni marudio baada ya
baadhi ya maeneo katika mitaa ya manispaa ya Iringa kushindwa kufanya
uchaguzi huo kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza ikiwemo
kukosekana kwa baadhi ya vifaa ambapo jumla ya mitaa 10 inarudia
kuchagua wenyeviti wa mitaa na wajumbe wao na mitaa mingine 9 inarudia
uchaguzi wa wajumbe baada ya wajumbe hao kugona kwa idadi ya kura.
0 comments so far,add yours