Chama cha mapinduzi CCM kimesema hakioni sababu ya suala la
waliohusika kusababisha dosari zilizojitokeza wakati wa zoezi la upigaji
kura kuundiwa tume au kuchunguzwa wakati wanajulikana, badala yake
wachukuliwe hatua, huku kikieleza kusikitishwa na mapungufu
yaliyojitokeza ambayo wamedai yalitokana na uzembe wa watendaji
wachache.
Katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho Bw Nape Nnauye ameyasema
hayo jijini Dar es Salaam ambapo amesema wakati umefika utaratibu wa
kuunda tume kila jambo ufe kwani ni matumizi mabaya ya fedha na mwisho
wa siku zinaleta ripoti machungungu ya jambo yakiwa yameisha hivyo
haifanyiwi kazi tena huku akielezea namna CCM ilivyofanya vizuri katika
uchaguzi wa serikali za mitaa.
Aidha kwa mara ya kwanza Bw Nape amevipongeza vyama vya upinzani
kwa hatua vilivyofikia lakini akadai kuwa kwa umri waliofikia tangu
vianzishwe hapa nchini havikupaswa kuwa hatua vilivyopo hivi sasa bali
walitakiwa kuwa mbele zaidi huku akivitaka kutekeleza yale yote
waliyoahidi kwa wananchi waliowapa dhamana na kuongeza kuwa furaha ya
CCM ni kuona mfumo wa ushindi unakuwa.
0 comments so far,add yours