JKT huandikisha vijana wa kujitolea
kutoka mikoa yote ya hapa nchini kila mwaka. Utaratibu unaotumika ni kwa
JKT kuandika barua kwa wakuu wa Mikoa na kuanisha nafasi ambazo mkoa
umetengewa.
Baada ya Mkoa kupata barua kutoka kwa
Mkuu wa JKT na idadi ya nafasi za vijana waliopangiwa kujiunga. Mkoa
hugawa nafasi hizo kulingana na wilaya zake. Pia wilaya zinatakiwa
kupeleka katika tarafa, kata na vijiji. Mara nyingi uongozi wa wilaya
hubandika tangazo la nafasi hizo katika ubao wao wa matangazo. JKT
hutangaza nafasi za kujiunga na jeshi hilo kupitia vyombo vya habari vya
Serikali na biafsi kwa nia ya kuharakisha taarifa kuwa. kia wananchi
hasa vijana. Usaili wa awali hufanyika chini ya Kamati za Ulinzi na
Usalama za Wilaya wanakotoka vijana hao, baadaye hufanyika mkoani, ili
kupata idadi ya vijana wa mkoa mzima.
Zoezi hilo linapokamilika mikoani, JKT
hutuma timu za maafisa na askari kutoka Makao Makuu ya JKT kwa ajili ya
kuhakiki vijana waliosailiwa katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Vijana
hupimwa afya zao na kusafirishwa katika vikosi vya JKT.
Kabla ya kuondoka timu za usaili kutoka
JKT hufanyiwa semina na kuelekezwa jinsi ya kubaini udanganyifu wa vyeti
bandia vya kuzaliwa na shule. Mhariri Mkuu wa Jarida la Vijana Leo
alikuwa ni miongoni mwa watu walioshiriki usaili mkoani Ruvuma. Vijana
wa mkoa huo walitoka katika Wilaya za Songea Mjini, Vijijini, Namtumbo,
Mbinga na Tunduru na kukusanyika Makao Makuu ya Mkoa wa Ruvuma. Vijana
hao walikuwa na shauku ya kupata nafasi ya kujiunga na JKT.
0 comments so far,add yours