Kufuatia kuvuliwa vyeo vya uongozi Mheshimiwa Zitto Kabwe kutokana na tuhuma mbalimbali, Msanii wa muziki Afande Sele ambaye ni mwanachama wa CHADEMA ameeleza ni kwa jinsi gani swala hili lilivyokuwa ni changamoto kubwa kwa chama chake hicho.

Afande Sele amesema kuwa, viongozi wa juu wa chama hicho wanatakiwa kuangalia wananchi wa chini kabisa wanaathirika vipi na suala hili na pia kutokuchukua maamuzi kwa kushirikishana watu wachache tu.

Vile vile Afande Sele pia ameonya viongozi hao wa juu kuhusiana na swala zima la uchu wa madaraka ili kukiimarisha chama zaidi.

Hata hivyo, licha ya maneno haya mazito, Afande Sele amesisitiza kuwa hawezi kukihama chama hicho kutokana na kuwa yeye ni muumini mkubwa wa sera zake

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours