Mratibu
wa matembezi hayo Bw, Matukio Chuma akiongea na waandishi wa habari
kwenye ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam wakati
akizindua matembezi yajulikanayo kama, Matembezi ya Nchi Yangu Wajibu
Wangu, yanayo tarajiwa kuanza, Januari 11-2014 kuanzia jijini Dar es
Salaam hadi Mkoani Morogoro matenzi hayo ya kilomita (200km), ambayo
yatachukua siku kumi 10,lengo la matembezi hayo kuhamasisha kila
Mtanzania kuamua kuchukua hatua kujikwamua kimaisha.
Ni
changamoto inayotolewa mbele ya Watanzania,kukumbuka maana halisi ya
uzalendo kujitoa mhanga kuweza kufanyikisha maendeleo yao wenyewe kwa
kujishughulisha na kujibidisha katika Nyaja mbalimbali kwa manufaa ya
Taifa,kujitolea kuanzia ngazi ya kaya mpaka taifa,kuacha kulalama tu
kuwa serikali haijawafanyia moja ama mbili lakini wao wenyewe kutambua
mchango wao kama Watanzania na wajibu wao kama wananchi, kubwa zaidi
kujivunia nchi iitwayo Tanzania kwa yale mema na adimu yaliyopo na
kurekebisha palipo na kasoro kwa moyo mmoja bila kujali itikadi,imani,
asili ama mtizamo miongoni mwetu, Tanzania,kwa nini Dar es Salaam mpaka
Morogoro.Dar es Salaam imendelea kuwa kituo kikuu cha shughuli nyingi za
kiuchumi, kiserikali na vilevile ni mkoa ulio na watu wengi zaidi
Tanzania, ta kribani milioni mbili na nusu (2.5mil) kawa mujibu wa sensa
ya watu ya mwaka 2002, wakati Morogoro ina watu wasiofika laki tatu tu,
na kwa ukuaji wa asilia 4.39 kawa mwaka inaweka pia kuwa ya watu barani
Afrika na tisa duniani, hii inawakilisha tofauti kubwa sio tu kwa idadi
lakini ya ukuaji, upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii, ukuaji wa
kiuchumi na vilivile hali ya kipato na fursa za iuchumi” alisema Chuma.
Mratibu
wa matembezi hayo Bw. Matukio Chuma akiwaonyesha waandshi wa habari
vazi litakalotumika kwenye matembezi hayo (kushoto), Mratibu wa
matembezi hayo Carren Mgonja.
Waandishi wa habari wakishuhudia uzinduzi huo.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM).
0 comments so far,add yours