Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepangwa katika kundi linaloonekana kuwa ni gumu.

Tanzania wako kundi A la michuano hiyo, michuani inayoshirikisha timu zilizo Ukanda wa Kusini mwa Afrika huku Stars ikishiriki kama timu alikwa.

Kwenye droo iliyofanyika jijini Lusaka, Zambia, siku ya Ijumaa, Taifa Stars imepangwa pamoja na
Namibia,  Mauritius, Swaziland. Ambapo mshindi wa kundi hilo ana uwezekano wa kukutana na Afrika Kusini katika hatua ya robo fainali.


Mechi ya Kwanza Taifa Stars watacheza na Swaziland mnamo tarehe 6 Julai, kisha Stars itakutana na Mauritius Julai 8 jijini Lusaka.

Stars watacheza mechi za mwisho za makundi dhidi ya Namibia tarehe 10 Julai kwenye mji wa Kabwe.

Stars ambayo kwa sasa ipo kwenye kiwango cha kuridhisha, wakifanikiwa kufika hatua ya robo fainali watakutana na Bafana Bafana ambao ni mabingwa mara tatu wa michuano hiyo.


Kila la heri Taifa Star.............
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours