Kuna mambo ambayo usipoyajua na kuyaishi katika maisha yako,yanatosha kabisa kukufanya uwe ni mtu ambaye kila siku utajikuta haupigi hatua kama ambavyo unatamani.Ingawa kila siku ni muhimu ila kila wakati unapoanza wiki mpya katika maisha yako ni muhimu sana kuzingatia kuwa kuna mambo ya msingi ambayo lazima uyafanye kwani kwa kutokuyafanya yanaweza yakawa sababu ya kutosha kukufanya kufeli bila kutarajia.

Watu wote waliofanikiwa kutimiza malengo, wamejiwkea mambo fulani ambayo walikuwa wanayafanya.Mambo haya na wewe ukianza kuyafanya utaanza kupata matokeo tofauti nayale ambayo umekuwa ukiyapata huko nyuma.Hii inaitwa kanuni ya kichocheo na matokeo.Ambayo inasema,kama ukifanya kile ambacho wanaotimiza malengo yao huwa wanafanya basi utapata matokeo ambayo wamekuwa wanayapata.Leo nataka tuangalie mambo 3 ambayo watu wanaofanikiwa huwa wanayafanya wanapoanza wiki yao:
Jambo la kwanza kabisa huwa wanaanza siku yao mapema sana tofauti na watu wengi.Kumbuka kuwa baada ya mapumziko ya mwisho wa wiki(weekend) kila mtu atajaribu kutumia siku ya kwanza ya wiki kukimbizana na mambo yaliyobakia kuwa viporo.Hii inaamisha kuwa ni jambo la kawaida sana kukuta kwenye email yako kuwa na email nyingi,ni jambo la kawaida sana kukuta kuwa unapigiwa simu nyingi,ni kawaida pia kukuta watu wengi wanapanick na kuwa na stress za hali ya juu siku ya jumatatu.Unapoanza siku yako mapema unajihakikishi kuwa utaitawala wiki yako na utajiepusha na presha na stress zisizo na sababu.Hii inamaanisha kuwa muda ambao wengine watakuwa ndio wanaanza kazi wewe tayari utakuwa umeshafanya mambo kadhaa nahii itakuepusha sana na kukimbizana kusiko na sababu.
Jambo la pili ni kuipangilia wiki yako nzima.Watu wanaofanikiwa sio tu huwa na malengo makubwa ya mwaka ama mwezi,bali pia hujiwekea maengo ya wiki.Ni muhimu kujiuliza na kuamua kuwa ni malengo gani ambayo ni makubwa kwenye maisha yako na ambayo ungependa kuyatimiza.Hii itakusaidia kujua namna ya kujipanga,watu wa kuwatafuta mapema,lakini pia kuhakikisha kuwa haujingizi katika majukumu ambayo siyo ya lazima na sio ya muhimu kwa ajili ya kesho yako.Kabla haujaivamia wiki yako,jitahidi sana kuitazama kuanzia mwisho kuja mwanzo na upate majibu thabiti ya mambo muhimu ambayo haswaa uantaka kuyafanikisha na kuyakamilisha wiki hii.Kumbuka mafanikio yako kwa mwezi huu yatategemea zaidi namna ambavyo utaitumia wiki yako ,Kwa maneno mengine usipotumia wiki vizuri utakuwa umetumia mwezi wako vibaya na utaishia kuwa na mwaka mbaya kabisa.
Jambo la tatu ni kuhakikisha kuwa unafanya kitu fulani kukusogeza katika malengo yako makubwa kwa mwaka huu.Kumbuka kuwa tabia yako ya kufanya kila siku kitu fulani hata kama ni kidogo ndio hupelekea kukufanya baadaye uwe umefanikiwa katika mambo makubwa.Kuna kanuni inaitwa kanuni ya dakika mbili(Two Minutes Rule),kama haujaisoma hii nashauri uitafute hapa kwenye website hii na usiome itakusaidia sana.Ila cha muhimu zaidi katka jambo hili la tatu ni kuhakikisha kuwa wiki hii haiishi kabla haujafanya kitu fulani kuhusiana na ndoto kubwa za mwaka huu,Je unataka kujenga,unataka kuanza shule,kuanza biashara,kubadilisha kazi n.k kwa chochote kile uanchotaka kukipata mwaka huu jaribu kutafuta kitu kidogo ambacho utakifanya na kitakusogeza kule ambako unataka kwenda.Wakati mwingine kitu ambacho unatakiwa kufanya hakihusishin pesa bali kinahusisha kutafuta taarifa tu ama kuonana na mtu fulani.Kwa vyovyote itakavyokuwa jitahidi sana kufanya kitu fulani kuhusiana na ndoto yako kubwa kabla wiki hii haijaisha.Ukifanikiwa nitafurahi sana ukinishirikisha.
Unaweza kushare makala hii pia na wengine ili iwasaidie kufikia malengo yao.Nakutakia wiki ya ushindi.
See You At The Top

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours