KOCHA wa timu ya Manchester United, Jose Mourinho, amesema
ataendeleza utamaduni wa kupongezana kwa kumwalika mpinzani wake, Kocha
wa Manchester City, Pep Guardiola, glasi ya mvinyo ofisini kwake
baada ya mchezo wao wa ‘Manchester Derby’ utakaochezwa kesho uwanja wa
Old Trafford.
Kocha hao wa zamani wa Barcelona na Real Madrid, wapo katika presha ya kufanya vizuri katika mchezo huo ambao utawakumbusha uhasama wao wa zaidi ya miaka 20 tangu wakiwa pamoja katika kabu ya Barcelona.
Akiwa katika mkutano na waandishi wa habari jana jijini Manchester, Mourinho alisisitiza mchezo huo hauna uhusiano wowote na makocha hao badala yake utakuwa wa kuonesha uwezo kwa wachezaji wa timu hizo. Hata hivyo, wakati Guardiola akiulizwa kama angekuwa na mlo na Mourinho, kocha huyo alipendekeza jambo hilo lingetokea bila ya wao kupanga.
Katika mkutano huo, Mourinho alionesha kusikitishwa na uadui uliokuwapo baina yao na kuamua kumwalika mpinzani wake baada ya mchezo huo.
Guardiola hadi sasa bado hajaamua kukubali mwaliko huo ambao utamkutanisha na kocha ambaye wamekuwa katika upinzani mkali zaidi kwa sasa.

0 comments so far,add yours