Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini–CTI,ulioambatana na kongamano kuhusu namna ya kuiharakisha Tanzania kuwa ya Viwanda.
Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Ukanda Maalum ya Uwekezaji –EPZA Mhandisi Joseph Simbakali,Waziri huyo amesema serikali ya awamu ya tano imejipanga vizuri kuondoa vikwazo vya uwekezaji,ikiwemo ukosefu wa maeneo ya kuweka viwanda.
Mapema Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini–CTI Dr Samwel Nyantahe alisema ukuaji wa sekta ya viwanda nchini bado ni mdogo,lakini inatoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya taifa,licha ya kukabiliwa nachangamoto mbalimbali, ikiwemo gharama kubwa ya kuanzisha biashara,kodi nyingi,ukosefu wa nishati ya uhakika,wana matumaini makubwa kuwa serikali itayatatua.
Akichangia hoja Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania-TPSF Dr Reginald Mengi amesema Tanzania itaweza kuendelea kiviwanda suala la kodi litasimamiwa vizuri, na kusisitiza kuwa ukwepaji mkubwa wa kodi na ushuru uliochochewa na uongozi mbaya ndio uliosababisha viwanda vingi vifungwe nchini katika miaka ya 80 na 90.
Akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo Mhadhili wa Chuo kikuu Dar es salaam Prof.Lucian Msambichaka alisema maendeleo ya haraka ya viwanda nchini yatapatikana kwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa,kuwa na sera sahihi, na utashi wa kisiasa na ushirikishwaji wa wadau wote katika
0 comments so far,add yours