Mashirika mbalimbali na watanzania
kwa pamoja wameombwa kuwa na utamaduni wa kuchangia na kuboresha shule
maalumu ambazo zina walemavu wa ngozi ,badala ya kusubiri matukio ya
uvamizi kutokea na kuanza kuchukuwa hatu ,kwa kufanya hivyo kuta saidia
walemavu wa ngozi kupata elimu bila ya kuwa na wasiwasi ya kuvamiwa na
baadhi ya watu wenye nia mbaya.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Vicent Kone amesema hayo katika
hotuba yake iliyo somwa na mkuu wa wilaya ya Singida, Bwana Said
Amanzi katika hafla ya kukabidhi mradi wa uboreshaji wa miundombinu
rafiki kutoka shirika la Koica la nchini korea,na kusema kuwa mashirika
kutoka mataifa mengine wame weza kuchangia na sisi watanzania
inatubidi kuchangia kwani jukumu la kuwalinda walemavu wangozi ni ni la
watanzai wenyewe na kuhakikisha wana pata ulinzi na elimu kama watu
wengine.
Kwa upande wake meneja mradi wa kujitolea kutoka shirika la Koica
nchini korea Bi. Park Jieun amesema mradi wa uboreshaji wa miundombinu
katika chuo cha ufundi na marekebisho kwa watu wenye ulemavu sabasaba
umegarimu zaidi ya shilingi milioni arobaini na mbili kwa ajili ya
kuboresha mazingira ya chuo kwa kujenga mabweni,matanki ya maji na
kuwasaidi walemavu ili waweze kuishi kama watu wengi ambao siyo
walemavu.
Awali mkuu wa chuo cha ufundi na marekebisho kwa watu wenye
ulemavu cha sabasaba Bi. Fatuma Malenga ameiomba serekali kuangali
uwezekano wa kukijengea uzio chuo na kuweka vivuko maalumu pamoja na
alama katika barabara ambayo ipo karibu na chuo ili kuwawezesha wenye
ulemavu wa ngozi na walemavu wengine kuishi katika mazigira salama.
0 comments so far,add yours