WAUZA MAFUTA WAFUNGIWA DAR KWA KUDANGANYIFU

WAKALA wa Vipimo, Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, imefungia vituo vya kuuza mafuta rejareja viwili kati ya sita baada ya kubaini kutoa huduma kwa njia ya udanganyifu kwa kuwaibia wateja huduma hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi  wa Wakala mkoani humo, Stella Kahwa alisema zoezi hilo limeanza jana na kwamba vituo viwili kati ya sita vimefungiwa baada ya kubainika vinatoa huduma kwa udanganyifu. "Matunda ya ziara ya ukaguzi wa mashine katika vituo vya mafuta tumefanikiwa kubaini vituo viwili (majina tunayahifadhi) tumevifungia kwasababu vinawapunja wateja.Kwa wale tuliowakuta na makosa haya watalipa faini kwa mujibu wa sheria zao na ikilizimu wataburuzwa mahakamani". Katibu Mkuu wa Umoja wa Wauza Mafuta ya rejareja (TAPSO) Tino Mmasi, alisema amesikitishwa na tukio la wafanyabiashara hao kuwapunja mafuta wananchi.

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours