Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk Reginald Mengi ameyasema hayo
jijini Dar es salaam wakati akikabidhi ruzuku ya shilingi milioni 10
kwa mshindi wa kwanza kwa Mwezi Januari , Bw. Frederick Shayo, wa
shindano la wazo la biashara analoliendesha kupitia twita yake kwa mwezi
Januari.
Akikabidhi zawadi hiyo Dr Mengi amewataka vijana na wananchi
kubadili fikra na kuamini kuwa kwa kutumia fursa na raslimali za taifa
wanaweza kubuni mawazo bora ya kufanya ujasiriamali utakaowawezesha
kujikwamua kiuchumi na kusisitiza kuwapuuza watu wanaodai kuwa Tanzania
haihitaji mamilionea.
Dr Mengi pia amewazawadia shilingi milioni moja kila mmoja
washiriki tisa waliofanikiwa kuingia kumi bora. Washindi hao ni Jesse
Temba, Charles Kapondo, Gerald Nyaisssa, George Rashid, na Otaigo
Elisha. Wengine ni Alphonce Mallya, Japhet Bachu, Kibanga Omari, na
Emmanuel Buberwa.
Wazo la mshindi wa kwanza lilikuwa kukarabati majokofu mabovu
kuyageuza kuwa viatamishi rahisi vinavyotumia umeme mdogo kwa ajili ya
wafugaji wa kuku.
0 comments so far,add yours