Taasisi ya Sekta Binafsi nchini -TPSF imeanzisha Mfuko Maalum wa kuwawezesha wanawake kugombea ubunge wa kuchaguliwa.
Uanzishwaji wa mfuko huo jijini Dar es salaam ni matokeo ya Mkutano
wa pamoja wa mashauriano baina ya TPSF na Wabunge Wanawake Wenye
majimbo nchini, uliokusudia kutafuta namna ya kuwawezesha wabunge
wanawake kushiriki na kushinda majimbo katika uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza katika mkutano huo Mbunge wa Hanang, ambaye pia ni
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary
Nagu amesema wanawake hawana budi kuwania nafasi za ubunge wa
kuchaguliwa, na kusisitiza kuwa ili harakati zao zifanikiwe ni lazima
ziungwe mkono na wanaume.
Mapema Mwenyekiti wa TPSF Dr. Reginald Mengi aliwahamasisha
wanawake nchini kujiamini kuwa wanaweza kufanya makubwa, iwapo harakati
zao za kupigania usawa zitawashirikisha pia wanaume.
Kuhusu Mfuko huo Dr Mengi amesema mtaji wake wa kuanzia utakuwa wa
kiasi cha shilingi milioni 100, ambapo jumla ya shilingi milioni 19.5
ziliahidiwa kuchangwa na wanachama wa TPSF waliohudhuria mkutano huo.
Wakati wa mkutano huo Baadhi ya wabunge wanawake na wanachama wa
TPSF waliotoa maoni mbalimbali kuhusu namna ya kuendeleza ushirikiano
baina yao.
0 comments so far,add yours