Serikali mkoani Singida imewaagiza wakurugenzi watendaji wa
halmashauri za wilaya pamoja na wakuu wa wilaya wote mkoani Singida,
kuhakikisha wanafuatilia miradi inayo anzishwa na iliyo kwisha anza
kufanya kazi, ili miradi hiyo iwe endelevu na kuwa saidia wananchi,
tofauti na sasa miradi mingi imekuwa haiendelei.
Akishukuru kwa niaba ya wakuu wa wilaya sita mkoani Singida
waliopewa mashine hizo, kiongozi wa wakuu wa wilaya mkoani Singida
mwalimu Queen Mlozi ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Singida,
amemuhakikishi mkuu wa mkoa mashine hizo pamoja na kuwapatia ajira
vijana, zitafanya kazi ya kufyatua matofali bora na kufanikisha kwa
kiwango kikubwa opereseni ya ondoa nyumba zilizo ezekwa kwa udongo
maarukwa jina tembe
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk .Parseko Kone ametoa agizo hilo wakati
alipokuwa akiwakabidhi wakuu wa wilaya mashine ishirini nanne za
kufyatulia matofali ( intetlocking blocks ) zilizo tolewa na shirika la
nyumba la taifa kwa ajilia ya kusaidia makundi ya vijana kujiajiri.
Awali akiongea kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa shirika la nyumba la
taifa, meneja wa NHC mkoani Singida Bwana Ladislaus Bamanyisa amesema
shirika la NHC limelenga kupunguza tatizo la makazi hapa nchini ifikapo
mwaka elfumbili na kumina tano kwa kujenga nyumba za beinafuu nchi
nzima, pia mashine hizo zina lenga kupunguza tatizo la ajira kwa vijana
hapa nchini.
0 comments so far,add yours