Mmoja
kati ya wafanyabiashara wakubwa wa nchini Marekani mwenye asili ya
Afrika Dr.Robert Shumake amekubali kuzileta treni za kisasa katika jiji
la Dar es salaam ili kusaidia kutatua kero ya usafiri katika jiji hilo
ambapo anatarajia kutumia zaidi ya shilingi Bilioni arobaini kufanikisha
hilo muda wowote kuanzia sasa.
Akizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano ya uletaji wa
treni hizo Dr.Shumake amesema anatarajia treni hizo zitafanya kazi saa
ishirini na nne na anaisubiri serikali ya Tanzania imalize tathmini ya
gharama za mradi huo na yeye aweze kutoa fedha za kuufanikisha.
Naye waziri wa uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe amesema treni hizo
zitafanya kazi kati ya Stesheni na Pugu na zitatumia miundombinu ya reli
iliyopo ila kutakuwa na ujenzi wa reli zingine katika baadhi ya sehemu
kuruhusu treni kupishana.
0 comments so far,add yours