Katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni
Sefue amekiri kuwepo kwa mapungufu katika mfumo wa ufuatiliaji wa
tathmini ya fedha na rasilimali za serikali hali inayochangia kuongezeka
kwa vitendo vya rushwa na utendaji mbovu katika idara na taasisi za
serikali kwenye utoaji huduma kwa umma huku miradi mingi ya maendeleo
hasa kutoka kwa wahisani kusitishwa kwa sababu ya vitendo hivyo.
Balozi Sefue anabainisha hayo katika mkutano wa faragha wa makatibu
wakuu manaibu katibu wakuu wa wizara na makatibu tawala wa mikoa ambapo
amesema mapungufu hayo kwa kiasi kikubwa yanachangia kuzorotesha utoaji
huduma kwa umma pamoja na kukwamisha shughuli za maendeleo na kuonya
kuwa serikali imechoka kuvumilia matukio hayo na kiongozi yeyote
atakayekosa dhamira ya kuyakomesha atawajibishwa.
Balozi Sefue pia amesema katika kuhakikisha viongozi wanawajibika
ipasavyo kwa jamii serikali hivi sasa inafanya upembuzi yakinifu wa
kuanzisha kituo cha tathmini ya uongozi ili utumishi wa umma uwe chachu
ya maendeleo ya taifa licha ya mpango huo kuonekana kupigwa na baadhi ya
viongozi.
Awali katika mkutano huo mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi
amewataka watumishi wa umma kuzingatia welendi katika kuteleleza
majukumu yao badala ya kusubiri kusukumwa na matamko au maagizo kutoka
ngazi za juu za uongozi kama ilivyokuwa hivi sasa kwa agizo la rais la
ujenzi wa maabara tatu katika kila shule ya sekondari.
0 comments so far,add yours