Moto mkubwa uliotokozea wakati wa jioni umeteketeza kabisa moja kati
ya nyumba mbili za mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar Naushad Mohamed na
kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.
Moto huo uliutokozea eneo la Beitras Njekidogo ya
mjini Zanzibar ulianza wakati wa saa kumi jioni lakini pamoja na kikosi
cha zimamoto kufika kwa mudamfupi upepo mkali uliokuwa ukivuma
ulisababisha moto huo kuwa na kasi na kuweza kutekekteza nyumba hiyo
huku taarifa ya familia ikielezea chanzo cha moto huo umetokana na
hitilafu ya umeme.
Wakizungumza na ITV mmiliki wa nyumba hiyo Bw
Naushand Mohamed mohamec amesema moto huo ulikuja ghafla na yeye alikuwa
katika nyumba nyingine huku aksiema moto huo umeangamiza hati zake zote
za nyumba na nyingine za biashara huku mkuu wa opresheni wa kikosi cha
zima moto sasa wa zimamoto Suleiman amesema moto huo ulikuwa mkubwa.
Moto huo ulizua mtafaruku mkubwa huku umati wa watu
kujazana nje ya jengo hali iliyosababisha jeshi la polisi kuweka ulinzi
mkubwa ambapo polisi walilazimika kulinda nyumba hiyo ndani na nje
wakiwa na silaha.
0 comments so far,add yours