Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limewashushia kipigo baadhi ya wafuasi wa Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema na kutumia mabomu kuwatawanya wanachama waliokuwa wakijiandaa kufanya maandamano katika ofisi ya Chadema mtaa wa Ngoto mjini Morogoro.
Askari wajeshi la polisi walionekana kwa wingi
kuzunguka ofisi za Chadema za mjini Morogoro ambapo wafuasi wa Chadema
walikua katika maandalizi ya kufanya maandamano huku wakionekana na
mabango ya kupinga kuendelea kwa vikao vya bunge la katiba ambapo kabla
ya mandamano hayo baadhi ya vijana walipigwa na kisha kupakizwa katika
gari la jeshi la polsi ambapo baadhi ya viongzi wa Chadema wamelalamikia
jeshi la polisi kutumia nguvu huku wengine wakilalamikia baadhi vifaa
vya ofisi kupote wakati wa vurugu hizo.
Katika hatua nyingine baadhi ya askari wa jeshi la
polisi walitaka kuingia kwa nguvu katika ofisi za Chadema kuwachukua
baadhi ya watuhumiwa walio kuwa wakifanya vurugu ambapo walizuiwa na
viongozi wa Chadema na mambo yalikua hivi.

HAPO JUU PICHANI NI
Ndugu wa marehemu Ally Nzona akiwa amesimama kando ya mwili wa ndugu yake katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro, ambaye alifariki kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mjini Morogoro
0 comments so far,add yours