EPL: Matokeo ya Man City vs Arsenal haya hapa

Baada ya mapumziko ya takribani siku 14, hatimaye ligi kuu ya England imerejea tena leo kwa mchezo mkali kati ya Man City dhidi ya washika bunduki Arsenal.
Mchezo uliopigwa kwenye dimba la Emirates ulikuwa mkali na wa kusisimua kwa timu zote zikipoteza nafasi kadhaa za ushindi.
Matokeo ya mwisho ya mchezo yalikuwa sare ya 2-2.
Sergio Aguero alianza kuifungia City katika dakika ya 28, na mpaka mapumziko vijana wa Pellegrini walikuwa mbele kwa 1-0.
Kipindi cha pili kilianza vizuri kwa Arsenal na ndani ya dakika 15 tu Jack Wilshare aliisawazishia timu yake.
Dakika kadhaa baadae Alexis Sanchez akaongeza goli la pili, lakini furaha ya Arsenal ikadumu kwa muda mfupi baada ya Martin Demichelis kuisawazishia City kwa goli la kichwa kupitia kona ya David Silva.
Dakika chache kabla ya filimbi ya mwisho Man City walikosa makosa magoli kadhaa huku Samir Nasri akikataliwa goli baada ya kufunga akiwa offside.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours