UONGOZI wa Yanga ambao haukosekani kwenye mazoezi ya Taifa Stars yanayoendelea katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam imepiga bao jingine la maana kwa watani zao wa Msimbazi.
Imemsainisha kiungo mshambuliaji matata, Hassan Dilunga aliyetamba na Ruvu Shooting msimu huu ikiwa ni usajili wa pili katika dirisha dogo baada ya kumsainisha Juma Kaseja.
Agosti mwaka jana mmoja wa viongozi wazito aliyejiuzulu Simba, alimalizana na Dilunga na akapeleka jina lake kwenye Kamati ya Usajili ya klabu hiyo akiahidi kumlipa kila kitu mpaka mshahara kwa fedha yake ya mfukoni, lakini jopo hilo likamkataa mchezaji kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutaka kumkomoa kiongozi huyo.
Dilunga, ambaye alikulia kwenye timu ya vijana ya Ruvu Shooting, ni kiungo mshambuliaji na fundi aliyetamba kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara ambaye kwa mujibu wa mchambuzi maarufu wa soka, Edo Kumwembe Yanga imepata mchezaji wa maana na ambaye atakuwa na madhara kwa timu pinzani.
“Nimemfuatilia sana kwenye ligi ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kutawala kiungo, kukokota na kupenya anavyotaka, anatumia sana akili kuliko nguvu, mwepesi kugeuka halafu ana kasi nzuri, ni fundi wa pasi za mwisho na anajua kufunga mabao,”alisema Edo.
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa Yanga, Abdallah Bin Kleb ambaye habanduki kwenye mazoezi ya Stars, alithibitisha jana
Ijumaa kwamba wamemsainisha mchezaji huyo mkataba wa miaka mitatu ingawa Kocha wa Ruvu, Boniface Mkwasa alishtuka na huenda akakosa raha wikiendi hii yote kwavile
Yanga wamemgusa pabaya.
Simba na Azam FC zilikuwa zikimnyatia mchezaji huyo, lakini Yanga ikawazidi ujanja.
Abdallah Bin Kleb alisema; “Tunaendelea na harakati zetu za kuboresha timu, kama nilivyosema awali malengo yetu ni kupata timu iliyo bora Tanzania na Afrika, tulimsajili Juma Kaseja na sasa Hassan Dilunga. Tumemsainisha mkataba wa miaka mitatu na kuanzia sasa ni mchezaji wetu halali.”
Mwenyekiti wa Ruvu Shooting, Kanali Charles Mbuge alisema: “Kwa sasa niko mbali kijijini kwetu Musoma nimepumzika, sina taarifa hizo kwa undani.” Hata hivyo, Mbuge aliongeza kuwa, Dilunga alikuwa bado ana mkataba wa miaka mitatu na Ruvu.
Kocha Mkuu wa Ruvu, Boniface Mkwassa alisema: “Hata mimi nasikia tu, lakini kama kweli pengo lake ni kubwa kwa sababu yule tulimwandaa na kumpika hadi kuwa vile, kwa hiyo kumpata mbadala wake ni lazima afundishwe mwingine, pia jambo ambalo litachukua muda sana na kutugharimu.”
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours