KIUNGO mpya wa Manchester United, Paul Pogba, alikosolewa vikali na
mashabiki wa timu hiyo baada ya kushindwa kung’ara katika mchezo wa
‘Manchester derby’.
Mfaransa huyo hakuwa kwenye ubora wake, hivyo alishindwa kuinasua Man United katika kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa mahasimu wao Manchester City.
Kufuatia shutuma hizo, mchezaji mwenzake katika kikosi cha Man United, Zlatan Ibrahimovic, ameibuka na kumkingia kifua akimwambia awapuuze wanaomkosoa.
Ibrahimovic anaamini kuwa muda si mrefu Pogba atadhihirisha ubora wake na kuwanyamazisha wanaomponda.
Nyota huyo wa zamani wa PSG, amedai kuwa Pogba mwenye umri wa miaka 23 atafanya makubwa na ‘kuwashushua’ wale wanaomwona mzigo klabuni hapo.
“Paul Pogba anatokea katika kizazi kilicho bora pale Ufaransa,” alisema straika huyo raia wa Sweden.
“Timu yao ya taifa haikuchukua ubingwa wa michuano ya Euro, lakini kizazi chao kilikuwa kizuri na wataendelea kuwa bora na Paul akiwemo.”
Licha ya maneno hayo ya Ibrahimovic, bado Pogba ameshindwa kuthibitisha kile kilichowafanya Man United watoe dau lililovunja rekodi ya usajili la pauni milioni 89.
Mpaka sasa kiungo huyo hajafunga katika michezo mitatu ya Ligi Kuu England, ingawa kikosi chake hicho kinashika nafasi ya nne baada ya kushuka dimbani mara tatu.
Kwa upande wake, Ibrahimovic ambaye alitua bure klabuni hapo ameshapasua nyavu mara nne.
Kikosi cha Man United kinachonolewa na kocha, Jose Mourinho, kitashuka dimbani kesho kumenyana na Feyenoord katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Europa.
Siku tatu baadaye, Pogba na wenzake watakuwa ugenini kusaka pointi tatu mbele ya Watford katika mtanage wa Ligi Kuu England.

0 comments so far,add yours