Wananchi wa Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu wamemuomba Waziri Mkuu ,KASIM MAJALIWA kuwasaidia kuondoa mgogoro uliopo kati yao na mwekezaji wa kampuni ya Mwiba Holidings ambaye amekuwa akiwakamata wananchi na kuwapiga jambo walilosema ni unyanyasaji.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao Mbunge wa jimbo hilo,SALUM KHAMIS amemw ambia Waziri Mkuu kuwa mwekezaji hu y o amekuwa kero kubwa kwa wananchi wa Meatu hasa wanaoishi kando kando ya Pori la Akiba la Makao.
Mbunge huyo pia amemuomba Waziri Mkuu kupitia upya mikataba ya mwekezaji huyo ambayo amesema imejaa utapeli mwingi na kwamba wananchi wa Meatu wamechoshwa na uonevu huo .
Akijibu malalalmiko ya wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Stendi Mwanhuzi Waziri Mkuu,KASIM MAJALIWA amesema Serikali tayari kuwavumilia wawekezaji wanaonyanyasa wananchi .
Waziri mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,ELASTON MBWILO akutane na mwekezaji hiyo na ifikapo tarehe 11 mwezi huu ampe taarifa na kama itaonekana ni jipu basi litatumbuliwa.
Home
All
Wananchi wa Wilaya ya Meatu wamemuomba Waziri kuwasaidia kutatua mgogoro kati yao na Mwekezaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments so far,add yours