Wanafunzi zaidi ya 300 wa shule za msingi Masuguru na Muheza zilizopo wilayani Muheza wanalazimka kukaa kwenye Majanvi na mifuko aina ya Viroba,kufuatia shule hizo mbili kuwa na uhaba mkubwa wa madawati na kusababisha wanafunzi kushindwa kusoma kwa tija.
ITV imeshuhudia wanafunzi walioathirika na tatizo hilo huku wengi wao wakiwa wamekalia mifuko aina ya Viroba na kwenye Majanvi hatua ambayo imesababisha kushindwa kusoma kwa ufanisi wanapokuwa darasani sanjari na ukosefu wa vyoo kufuatia wanafunzi zaidi ya 1200 wa shule ya msingi muheza hawana tundu hata moja la choo na badala yake wanafunzi hujisaidia vichakani na wengine katika nyumba za majirani zilizopo katika eneo hilo.
Kulingana na changamoto hiyo benki ya nmb imesaidia kuwapunguzia adha wananfunzi hao kwa kuwapatia madawati 50 ambapo shule ya msingi muheza imesaidiwa madawati 25 na nyingine ya Masuguru imepata idadi kama hiyo ili kuwapunguzia adha wanafunzi kwa kukaa chini.
Kufuatia hatua hiyo mkuu wa wilaya ya Muhea Bibi.Esterina Kilas kabla ya kukabidhiwa madawati hayo amewataka wakazi wa wilaya hiyo kusaidia katika sekta ya elimu kisha kuwapongeza watendaji wa benki ya NMB kwa kuwapunguzia adha ya ukosefu wa madawa

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours