Mjadala wa bunge kuhusu mpango wa maendeleo wa serikali umechukua sura nyingine baada ya baadhi ya wabunge kutumia muda wao mwingi kuzungumzia mvutano wa kisiasa unaoendelea sasa huko visiwani Zanzibar ambapo wamesema kuna haja ya mgogoro huo kuangaliwa kwa jicho la karibu kwani unaweza kukiingiza kisiwa hicho matatani.
Mjadala huo ulisasabisha mwanasheria mkuu wa serikali kuingilia kati ili kuleta utulivu.
Mbali na suala hilo la Zanzibar wabunge wengine walitoa maoni yao kuhusu mpango uliowasishwa na waziri na kusema ambapo Mh Almas Maige mbunge wa Tabora kasikazini amesema pango ulipwa kuipa nguvu sekta binafsi kwa sabababu ndio muhimili mkuu wa uchumi.
Aidha Mh Abdalah Mtolea mbunge wa chama cha wananchi CUF amesema inashangaza kuona kuwa ni zaidi ya miaka 50 sasa bado tatizo la maji Dar es Salaam halijapatiwa ufumbuzi na mpango uliowasilishwa hautoi dira kamili ambapo Mh Stepheni Ngonyani mbunge wa CCM amesema kabla ya kutekeleza mpango huu serikali wamaliziye miradi ya mwanzo
0 comments so far,add yours