Kiongozi wa kanisa katoliki nchini
Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo amewataka wakristo kote nchni
kumuomba mungu aliepushe taifa na matukio ya ubaguzi, vita, ugaidi na
mauaji yanayotokea Duniani ikiwemo mauaji ya kikatili ya wanafunzi
waumini wa kikristo yaliyotokea katika chuo kikuu cha Garisa nchini
Kenya.
Akizungumza katika ibada ya Jumatatu ya Pasaka iliyohudhuriwa na
mamia ya wanachama wa shirikisho la kwaya katoliki nchni, Kadinali Pengo
pia amewataka wakristo nchini kumuomba mungu asafishe hali
iliyojitokeza nchini Kenya na kuwataka kuwawajasiri na kubaki katika
misimamo ya imaniya kikristo kwa kutamka ukweli iwapo hali hiyo
italazika kujitokeza.
Aidha kuhusu katiba inayopendekezwa,Padinali Pengo amesema kama
kiongozi wa Dini hawezi kurudia au kubadilisha kauli aliyokwisha itoa
kwa wananchi,kwani kufanya hivyo kutaweza kusababisha ugomvi ambapo
amewataka waumini wa kanisa katoliki kusambaza kauli hiyo kote nchni.
Awali kiongozi wa kanisa katoliki nchini Mwadhama Polycarp
Kadinali Pengo ametaka wananchi waachiwe wasome katiba inayopendekezwa
na kufanya maamuzi wenyewe.
0 comments so far,add yours