Baadhi ya waathirika wa mafuliko katika kijiji cha mwakata wilaya ya
kahama mkoani shinyanga wameladhimika kuifunga barabara ya isaka kahama
na kuathiri kwa muda mawasiliano katika nchi ya rwanda,burundi na uganda
wakishinikiza serikali kuwagawia chakula,magodoro,branketi.mahema na
shuka baada ya kunyeshewa na mvua usiku wakati vifaa vya misaada vikiwa
vimefungiwa kwenye magara hali iliyosababisha jeshi la polisi kuwatawa
na wananchi kwa mabomu ya machozi na kufungua njia ili gari ziendelee na
safari.
Naye mkuu wa mkoa wa shinyanga Bw.Ally Nasoro Rufunga amekabidhi
misaada hiyo kwa wenyeviti wa serikali za vitongoji na vijiji pamoja na
kutoa fedha zaidi ya shilingi milioni nne kwa kaya 14 ambapo kila
familia iliyofiwa imepatiwa kiasi cha shilingi laki tatu kama pole ya
rambirambi ya serikali ya mkoa wa shinyanga na kuahidi kusaidia zaidi
kadri misaada inavyopatikana.
Vurugu hizo zimedumu saa moja ambapo kundi la wananchi wenye
hasila wakiillamika kamati ya maafa kwa kushindwa kuwahudumia waathirika
kwa wakati hali iliyosababisha waathirika wanaolala nje kunyeshewa mvua
huku wakinamama wakila ani nguvu kubwa iliyoumika kutuliza ghasia
zilizosababisha watoto kupotea kutokana na mabomu ya machozi
yaliyotumika kutawanya wananchi waliofunga barabara.
Kufuatia vurugu hizo mbunge wa jimbo la msalala Mh.Ezekiel Maige
ameladhimika kufika kwenye eneo la tukio na kujionea hali halisi ambapo
amewasihi wananchi kuwa watulivu wakati akifanya mipango ya kuzungumza
na kamati ya maafa ili iweze kutoa vifaa vinavyolalamikiwa na
vigawiwekwa walengwa.
Alipotakiwa kujibu malalamiko hayo katibu wa maafa wilaya ya kahama
ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ushetu kahama
Bi.Isabela Chilumba amesema vurugu hizo zinasababishwa na wanasiasa na
kwamba kamati ya maafa imeba ini kunakundi la vijana kutoka vijiji
jirani wakivizia chakula na vifaa vya misaada.
0 comments so far,add yours