Mkuu wa mkoa wa tabora BW. RUDOVICK mwananzira, amesema vifo vya
akinamama na watoto vinaweza kuzuilika, kama kila mmoja atatimiza wajibu
wake, ambapo amemuagiza mganga mkuu wa mkoa huo kuvitolea maelezo vifo
hivyo kutokana na kupanda na kushuka kila mwaka na atabainika
aliyehusika hatua zichukuliwe dhidi yake.
Awali katibu tawala wa mkoa wa Tabora Bibi Kudra Mwinyimvua
akimkaribisha mkuu wa mkoa katika uzinduzi huo, amesema kuwa uwepo wa
mashirika binafsi na taasisi za dini zinayojihusisha na kupunguza vifo
vya akinamama ni msaada kwa serikali mkoani, ambapo ratibu wa vifo vya
akinamama na watoto kanda ya magharibi Bibi Mather Ndimbo akiwataka
jamii nzima kuguswa na changamoto hiyo
Bw. Rudovick Mwananzira anetoa kauri hiyo wakati akizungumza na
wadau wa afya mkoani Tabora, katika akizindua mpango mkakati wa
kupunguza vifo vya akinamama na watoto, pamoja na kutathimini maendeleo
ya kupunguza vifo hivyo ambapo amebainisha kushindwa kufikia lengo la
chini ya vifo theruthi mbili mwaka 2015,
Aidha amesema kuwa, lengo lililowekwa la kupunguza vifo kutoka
112/100,000, kufikia 90/100,000, mwaka 2013, halikufikiwa na matokeo ya
vikaongezeka mpaka 117,/100,000, 2014, na hivyo unahitajika uwajibikaji
ili kufikia lengo lililokusudiwa, na hatua za makusudi zichukuliwe
ikiwemo kuwajibishana.
0 comments so far,add yours